Msanii H Baba na mkewe Frola Mvungi wamefanikiwa kumpata mtoto wa kike jana jioni majira ya saa 12:30 katika hospitali ya Maria Stope iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Kama unakumbuka hapo awali H Baba alisema kama akifanikiwa kupata mtoto wa kike au kiume basi atampa jina 'Tanzanite' hatimaye amefanikiwa kumpata wa kike na kumpatia jina la Tanzanite.