Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe, Dkt. Sira Ubwa Mamboya, akizungumza na Ujumbe wa Maseneta wa Marekani waliofika Zanzibar kukagua miradi yao katika Wizara ya Afya Zanzibar, akitowa maelezo ya maendeleo ya miradi hiyo katika Sekta ya Afya. mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Jidawi, akimsikiliza Mmoja wa mjumbe wa Maseneta akizungumza katika mkutano huo wakati wakiwa katika ziara ya kutembelea miradi ya Afya inayofadhiliwa na Marekani Zanzibar.