![]()
Mrembo Wema Isaac Sepetu 'Beautiful Onyinye' akiwa na tuzo yake baada ya kuibuka Ijumaa Sexiest Girl 2013/14 ndani ya Dar Live usiku wa kuamkia leo.
![]()
Wema akiwashukuru mashabiki wake waliompigia kura na hatimaye kuibuka mshindi.
![]()
...Akiwapa tano mashabiki waliofurika Dar Live katika Sikukuu ya Pasaka.
![]()
Wema, Wema, Wema... mashabiki wakimshangilia 'Beautiful Onyinye' baada ya kutangazwa mshindi.
![]()
Mhariri wa Gazeti la Ijumaa lililokuwa likiendesha shindano la Ijumaa Sexiest Girl, Amran Kaima (kulia) akipozi na mshindi Wema Sepetu. Kushoto ni shabiki wa Wema.
![]()
Amran Kaima akielezea mchakato uliotumika kumpata mshindi wa Ijumaa Sexiest Girl.
![]()
Mashabiki wakiwa wamepagawa na shangwe za Dar Live.
![]()
Mratibu Mkuu wa kampuni ya Global Publishers, Luqman Maloto akiwakaribisha Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho na msanii Nikki wa Pili kukabidhi tuzo kwa mshindi.
![]()
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akiongea machache kabla ya zoezi la utoaji tuzo.
![]()
Msanii kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili akimtaja mshindi.
![]()
Wema Sepetu akiwa stejini baada ya kutangazwa mshindi.
![]()
Nikki wa Pili akimkabidhi tuzo ya Ijumaa Sexiest Girl, mrembo Wema Sepetu.
![]()
Wema akipozi na tuzo yake.
![]()
Wema akicheza wimbo wa Number One ulioimbwa na mpenzi wake Diamond Platnumz baada ya kutwaa tuzo.
![]()
Washereheshaji katika usiku wa Pasaka, Pamela Daffa na Benjamin Mwanambuu wakifanya yao stejini.
![]()
Said Fella (wa pili kushoto) akiwa na crew ya Madj ndani ya Dar Live.
![]()
Dogo Aslay akiwapagawisha mashabiki wa burudani waliofurika ndani ya Dar Live.
![]()
![]()
...Aslay akijiachia na shabiki wake aliyepanda stejini kumpa sapoti.
![]()
...Akimchombeza shabiki mwingine aliyepanda stejini.
![]()
Kundi la TMK Wanaume Family likifanya vitu vyao stejini.
![]()
Mhe. Temba akiwarusha mashabiki wa Dar Live.
![]()
Chegge Chigunda 'Mtoto wa Mama Said' akizikonga nyoyo za wana Dar Live.
![]()
TMK Wanaume Family wakizidi kulishambulia jukwaa la Dar Live la kupanda na kushuka.
![]()
Wana Hip hop wa Kundi la Weusi, Joh Makini (kulia) na G-Nako wakiwapa raha mashabiki.
![]()
Mashabiki wakifuatilia shoo ya Weusi.
![]()
Joh Makini kazini.
![]()
G-Nako akiwadatisha wapenzi wa Hip hop. GPL