Quantcast
Channel: MWINYI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3319

JINSI MWILI WA MAREHEMU SAMWEL P. KITULA ULIVYOAGWA CBE DODOMA.

$
0
0

Mnamo saa nane ( Mchana) mwili wa marehemu Samwel P. Kituli uliwasilishwa chuo cha CBE Dodoma kuagwa na wanafunzi wenzake. Baada ya hapo mwili huo unasafirishwa kuelekea mkoani kwao marehemu.

Huu ni upande wa familia ya marehemu mbele yao kukiwa kuna sanduku lililohifadhiwa marehemu Samwel P. Kituli, aliyepatwa na umauti tarehe ya kuamukia December 26,2013 chanzo cha umauti huo ikiwa ni uvimbe wa Ini kwa mjibu wa Madaktari baada ya vipimo kubainisha tatizo hilo.


Kwaya ya Mtakatifu Cecilia kutoka CBE Roman Catholic iliyoshiriki kwenye kuaga mwili wa marehemu

Watu wakipigwa butwaa kwa msiba huu

Wafanyakazi wa chuo hiki nyuso zao zikiwa ni zahuzuni kwa sababu ya kipindi kigumu kilichojitokeza, ikiwa siku ya leo tena tarehe 27/12/2013 wameondokewa na mfanya kazi Marehemu Selina Makindi hali ikiwa tete kweli.
eeeeh Mungu tusaidie

Wadau mbali mbali waliohudhulia
Mapadree wa kiongoza misa takatifu ya marehemu Samwel

Hawa ni viongozi kushoto ni Raisi wa (COBESO) Mhe, Remidius Emmanuel na kulia ni Mshauri wa wanafunzi

Marehemu akinyunyiziwa maji ya baraka kwa ishara ya imani yake aliyebatizwa kwa maji ya baraka

Sala kwa marehemu


Ndugu na jamaa wakiwa na majonzi mazito

Katibu mkuu kiongozi Mhe, Dickson Msigwa kutoka serikali ya wanafunzi akisoma wasifu/historia fupi ya marehemu

Rais wa (COBESO) Mhe, Remidius M. Emmanuel alipopata nafasi ya kusimama na kuzungumza,

''Ilikuwa tarehe 25/12/2013 nilipopata taarifa ya Bw. Samwel anaumwa nlienda kumuona lakini nikamkuta mke wake akaniambia amelala basi niliondoka nakutarajia kesho nirudi tena na marafiki zetu kumuona. Muda wa saa nane usiku nilipokea simu na kuambiwa Samwel amepoteza maisha.

Samwel alikuwa nitegemeo letu kama serikali akiwa ni mshauri wetu nitamkumbuka Daima'' maneno ya Rais wa (COBESO).
Mshauri wa wanafunzi Mhe, L. Sikato alipopata nafasi ya kusimama '' Napongeza serikali iliyopo madarakani kufanya vyema ikiwa nina mwaka wa 7 sijawahi kuona Serikali ya wanafunzi wanatoa Fedha kwenye mfuko wao na kuchangia, hizi pongezi ziende kwa Rais wa serikali ya wanafunzi Mhe, Remidius na timu yake nzima kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa, na huu uwe mfano mzuri wa kuigwa na serikali itakayo ingia madarakani awamu nyingine tena''
Chuo kimejitole sanduku la marehemu na kusafirisha mwili huo.

RAMBI RAMBI
Chuo - 200,000/=
Wafanya kazi - 72,000/=
COBESO - 50,000/=
Wanafunzi wote - 173,650/=
Jumla - 495650/=


Muda wa kuaga Rais wa COBESO akitoa heshima za mwisho kwa marehemu

Heshima za mwisho

Safari ya kuelekea

Mshauri wa wanafunzi Mhe, L. Sikato akiwa mstari wa mblele kupeleka mwili wa marehemu Samwel P. Kitula Ukelewe Mkoani Mwanza.
 Asante kwa kutembelea blog yangu, naomba ubonyeze HAPA ulike page yangu ya facebook ili uendelee kupata matukio mbalimbali ya hapa na pale.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3319

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>