
Nawazungumzia Mapacha wawili kutoka Nigeria yani Peter & Paul - (P-square) kuangusha show baabkubwa pamoja na wasanii wa hapa nyumbani kama vile Prof Jay, Ben Paul, Lady Jay Dee na wasanii wengine pale katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam leo usiku.
Kenedy The Remedy akizungumza na East Africa Radio leo amethibitisha kuwa ulinzi utakuwepo wa kutosha, ambapo pia milango ya kuingilia katika tukio itakuwepo takribani minane. Wahi tiketi yako katika matawi zinapopatikana.