Quantcast
Channel: MWINYI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3319

SERIKALI KUIMARISHA UDHIBITI WA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE NCHINI

$
0
0


Mratibu wa Taifa wa Mpango wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Upendo Mwingira KUSHOTO akiwaonesha waandishi wa habari Dawa za Kingatiba za Magonjwa yasiyopewa kipaumbele yaliyosambazwa katika wilaya 97 kupitia Bohari kuu ya Madawa. KULIA ni Afisa Habari Bi.Catherine Sungura wote kutoka Wizara hiyo, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari leo Jijini Dar es Salaam. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa akiwatambulisha kwa waandishi wa habari wawasilishaji toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika mzunguko wa pili wa Taasisi za Serikali kuongea na waandishi wa habari, KATIKATI ni Mratibu wa Taifa wa Mpango wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo Mwingira na KULIA ni Afisa Habari Bi.Catherine Sungura wote kutoka Wizara hiyo, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari leo Jijini Dar es Salaam.
************************************
Sera ya afya ina lengo la kuinua hali ya maisha kwa wananchi wote mahali popote walipo ikiwa mjini au vijijini kwa kupunguza maradhi na vifo kwa wananchi na kuongeza umri wa maisha yao kwa kuwa na afya thabiti kimwili, kiakili na kijamii. Vilevile ieleweke kwamba afya bora ni rasilimali kubwa kwa maendeleo ya kiuchumi na kiakili.

Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imejikita katika kuimarisha, kuboresha na kusambaza huduma za afya na ustawi wa jamii nchini, kwa kuzingatia Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi(MMAM-2007-2017),imejikita katika kudhibiti magonjwa yasiyopewa kipaumbele.Magonjwa yasiyopewa kipaumbele ni magonjwa ambayo yanaathiri jamii ya watu hususani wenye kipato cha chini wanaoishi katika maeneo duni, maeneo ambayo hata upatikanaji wa huduma za afya ni mgumu.

Magonjwa hayo ni pamoja na Matende na mabusha, Usubi, Trakoma, Kichocho, Minyoo ya tumbo,Homa ya malale,Kichaa cha mbwa,tauni,Tegu na mengineyo.Maambukizi ya Magonjwa haya yanatokana na kuenezwa na wadudu kama vile mbu, nzi na konokono. Udhibiti wa magonjwa haya unaelekezwa kwenye kinga tiba,usafi binafsi wa mazingira na udhibiti wa wadudu waenezao magonjwa hayo.

Athari za magonjwa haya yasipotibiwa mapema ni pamoja na saratani ya kibofu cha mkojo na ini,upofu,utumbo kujifunga na dalili za kifafa.Magonjwa haya husabababisha pia ulemavu wa kudumu hali ambayo inapunguza uwezo wa wananchi wetu kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya kiuchumi.

Magonjwa haya huathiri pia watoto na hivyo kupunguza mahudhurio ya watoto shuleni hatimaye maendeleo yao katika masomo kuathirika. Magonjwa na yanaongeza matumizi ya rasilimali chache tulizonazo katika kuyakabili kwa gharama kubwa mno. Pamoja na athari zote hizo, waathirika wa magonjwa haya wakabiliwa na unyapaa katika jamii.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imepiga hatua kubwa katika udhibiti wa magonjwa hayo kwa kuimarisha, kuboresha na kusambaza huduma za Mpango wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele kwa jamii zilizoathirika nchini. Katika mwaka 2012/2013, wizara kwa kuzingatia Mpango wa Taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele imefanikiwa kutekeleza yafuatayo:· Kuzindua rasmi Mpango Mkakati wa Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele (2012-2017).
· Kuongeza idadi ya wilaya zinazotekeleza mpango huu kutoka 76 mwaka 2011 hadi halmashauri 93 kati ya 155 yaani asilimia 60% halmashauri zote kwa nchi nzima
· Kutibu na kukinga watu milioni 15.4 kwa dozi million 36 za dawa za Mectizan, Albendazole, praziquantel na Zithromax.
· Kufanya Tathminini ya awali ya ugonjwa wa Trachoma katika wilaya 9. Matokeo yanaonyesha Wilaya 10 zilizofanyiwa tathmini hiyo hazihitaji kinga tiba i.e MDA · Uzinduzi wa kampeni ya ugawaji wa dawa katika jiji la Dar (kwa jamii) pamoja na Mwanza ( mashuleni).
Kwa kiasi kikubwa serikali imejitahidi kuboresha huduma za udhibiti wa magonjwa hawa kwa kusambaza dawa za kingatiba za magonjwa haya katika wilaya 97 kupitia Bohari kuu ya Madawa,kuwa na waratibu wa Mpango huu katika ngazi za Mkoa na wilaya.Waratibu hawa wanapatiwa Mafunzo na maelekezo ya utekelezaji wa mpango kila mwaka.Utekelezaji wa Mpango huu unafanyika katika ngazi ya wilaya na hivyo Halmashauri zote zilizoathirika zimeelekezwa kutenga rasilimali katika mipango yao ya Afya kupitia Muongozo wa CCHP.

Mwisho napenda kutoa wito kwa wananchi wote kumeza dawa hizi za Kingatiba kama wanavyoelekezwa na wataalam wakati wa Kampeni husika.Dawa hizi zimethibitishwa na shirika la afya duniani pamoja na mamlaka ya Chakula na dawa nchini kuwa ni salama na hazina Madhara yeyote.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3319

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>