Quantcast
Channel: MWINYI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3319

HAFSA KAZINJA KUURUDIA WIMBO WA GURUMO

$
0
0


Kutoka kushoto ni Mwanamuziki wa zamani wa miduara Omari Mkali , Hafsa Kazinja ( katikati) na Abdul Salvador.


IKIWA ni siku nne tu tangu gwiji wa muziki wa dansi ambaye kwa sasa anaimba nyimbo za kumtukuta mungu Cosmas Chidumule kutangaza mbele ya waandishi wa habari kutunga wimbo maalumu wa kumuenzi Muhidin Gurumo sasa Malkia wa mmuziki katika miondoko ya Zouk Hafsa Kazinja nayeye ametangaza kumwimbia mtafu huyo wa muziki wa dansi .

Kazinja ambaye kwa muda mrefu alikwa nje ya nchi nchini Marekani anasema amepania kuibuka upya katika fani huku akiwa na ingizo lake la kwanza kati ya kumi aliyoandaa kwa kuimba wimbo maarufu wa NUTA Jazz Band uitwao ´Nimuokoe Nani´ anauouleta hewani katika mahadhi ya Zouk.

Hafsa Kazinja anasema ameamua kurudi ulingoni kwa kutoa wimbo huo ili kumuenzi Gurumo ambaye amestaafu rasmi fani ya muziki baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka 53 huku akiwa na bendi mbalimbali nchini.

“Nimeamua kuimba wimbo huu wa ´Nimuokoe Nani ili kumuenzi gwiji huyu wa muziki kwani wakati yeye anastaafu na mimi ndiyo naibuka upya baada ya kukaa kimya kwa muda”, anasema Kazinja aliyetamba na wimbo wake wa “Presha” aliomshirikisha Banana Zorro.

Hafsa ameandaa wimbo huo wa Nimukoe nani” wimbo huo amerekodi katika studio za Omari Mkali inayofahamika kwa jina la OM Productions iliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam akisaidiana na mwanamuziki nguli, Abdul Salvador .

“Nafurahi kwamba wimbo nimeimba wimbo baada ya kupata baraka zote kutoka kwa mtunzi na mwimbaji wake Mzee Gurumo mwenyewe¨alisema Kazinja.

“Haikuwa rahisi kama inavyoweza kudhaniwa kwani baada ya kwenda kumuona nyumbani kwake alinifanyisha mtihani wa kuuimba wote kabla ya kuridhika maana alisema asingefurahi kuona wimbo wake unaimbwa hovyo hovyo na kuharibiwa ladha yake”, anasema kazinja, ambaye hivi sana anamalizia ngoma zake zingine tisa alizotunga mwenyewe, kabla ya kuvamia anga kwa mara ingine.

Hafsa anasema katika ukimya wake amekuwa akifanya utafiti na kujifunza kwa undani zaidi fani ya muziki, akipata mawaidha maridhawa toka kwa wanamuziki nguli ndani na nje ya nchi wakiwemo Gurumo, Omar Mkali, Abdul Salvador na Lokassa ya Mbongo wa Jmhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) aliyekutana na kufanya naye kazi alipokuwa ziarani nchini Marekani hivi karibuni.

Msanii huyu wa muziki wa kizazi kipya anasema ataitambulisha rasmi ngoma hii ya kumuenzi Gurumo katika tamasha la kumuenzi Gurumo lililopangwa kufanyika Oktoba mosi , 2013 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

“Natumaini wapenzi wa muziki watafurika kwa wingi kwenye tamasha hilo nami naahidi kuitendea haki ngoma ya gwiji huyo ya Nimuokoe nani hivyo wadau wa muziki wasikose kuja kujionea wenyewe jinsi siye wa kizazi kipya tunavyoweza kufanya kazi na wakubwa wetu wa kazi, anaongezea Kazinja ambaye pia anaandaa video yake pamoja na ya ngoma zake zingine mpya.

Mkongwe Abdul Salvador, ambaye alikuwa mmoja wa waanzilishi wa bendi ya Tancut Almasi iliyokua na maskani nyake mkoani Iringa iliyotamba na mtindo wake wa Fimbo Lugoda , anamtaja Kazinja mmoja wa wanamuziki wa kike waliojaaliwa sauti nzuri na kipaji cha hali ya juu hapa nchini.

“Kwa kuweza kuimba wimbo wa Gurumo na kupatia kisawasawa inadhihirisha kwamba Kzinja ni mwanamuziki aliyekomaa maana si mchezo kuimba nyimbo ya wakongwe kwa ufasaha kama alivyofanya Kazinja

“Hii inadhihirisha kwamba uwezekano wa kizazi kipya na cha zamani kufanya kazi pamoja ni mkubwa sana na sioni kwa nini isiwe hivyo”, anasema Salvador.

Omari Mkali, aliyetamba na bendi ya Chuchu Sounds, chini ya marehemu Yusuf Chuchu, naye anamwelezea Kazinja kama moja ya majembe ya muziki hapa nchini kwa upande wa kinamama, na kwamba anaweza kufika mbali endapo kama moto aliokuja nao upya atauendeleza.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3319

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>