
Mwanamke mmoja achomoka taya akipanua mdomo kung’ata ‘burger’.
Mwanamke mmoja nchini Uingereza amelazimika kwenda hospitali kuunganishwa tena taya yake baada ya taya hiyo kufyatuka mahali pake wakati akila ‘Burger’ ya vipande vitatu.
Mwanamke huyo Nicola Peatekutoka Ormskirk, Lancashire alijiumiza mwenyewe wakati akila mkate huo maarufu unaochanganywa na nyama, saladi na vitu vingine katika mgahawa wa Almost Famous ulioko Liverpool.
Peate mwenye umri wa miaka 25 amesema kuanzia sasa atakuwa makini na ukubwa wa kitu anachokula.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Idara ya Dharura ya Hospitali ya Royal Liverpool University Kathryn Clark uchomokaji wa viungo wa aina hiyo hutokea mara chache.
Peate amesema katika siku zijazo kama chakula anachotaka kula ni kikubwa basi ataomba kikatwe vipande vinavyowezekana kuingia mdomoni bila kuleta madhara.