Quantcast
Channel: MWINYI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3319

Dkt. Fenella akutana na wadau wa Filamu na kuzungumza nao.

$
0
0



Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Waziri Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na Viongozi wa Steps Entertainment (hawako pichani) wakati walipomtembelea ofisini kwake kwa mazungumzo juu ya maendeleo ya kazi za sanaa jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Waziri akitoa darasa kwa baadhi ya washiriki waliohudhuria kikao.



Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fissoo akichangia wakati wa kikao kati ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara na Steps Entertainment.



Moja ya viongozi wa Steps Entertainment Bw. Jairaj Damodaran akifafanua jambo wakati wa kikao na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara.



Baadhi ya viongozi walioshiriki katika kikao hicho wakimsikiliza Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Waziri Dkt. Fenella Mukangara (hayupo pichani) wakati akiwaelezea jambo wakati wa kikao jijini Dar es Salaam.



Mtaalum Mshauri Bw. Sanctus Mtsimbe akiomuonyesha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt Fenella Mukangara (hayupo pichani) moja ya kazi yake iliyopitia taratibu zote na ambayo hakimiliki ni yake mwenyewe.



Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamun Tanzania pamoja na Mkurugenzi wa Utamaduni Prof. Hermas Mwansoko wakisikiliza majadiliano wakati wa mazungumzo kati ya Steps na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara jijini Dar es Salaam.



Baadhi ya viongozi wa Steps wakimsikiliza Katibu wa Bodi wakati akielezea jambo wakati wa kikao na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara kilichofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO).

Na Benedict Liwenga-MAELEZO

WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara amekutana na wadau wa Kampuni ya Steps Entertainment na kuzungumza nao juu ya maendeleo ya Tasnia ya Filamu nchini. Ujumbe huo wa Steps ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu Bw. Dileshi Solanki

Katika mazungumzo hayo Dkt. Fenella amegusia masuala ya uharamia katika kazi za filamu nchini na kutia mkazo katika suala zima la maadili. Aidha Waziri ameeleza kuwa kuanza kwa urasimishwaji wa tasnia ya filamu na muziki unaoendelea kutekelezwa nchini kutasaidia sana kuondosha kazi zisizohalali.

Aidha, Dkt. Fenella amewashauri wadau wa tasnia ya filamu nchini washirikiane kikamilifu na Serikali katika kuendeleza na kukuza tasnia ya filamu na pia kuhakikisha wasanii wananufaika na jasho lao. Aidha ameeleza umuhimu wa kutoa elimu kwa wadau na umma kwa ujumla juu ya fursa nyingi zilizopo katika tasnia.

Kwa upande mwingine Waziri Dkt. Fenella ameshauri pia kuwe na majumba maalum kwa ajili ya kuonyeshea sinema ambayo yatakuwa yanazipa kipaumbele filamu za kitanzania pia amehamasisha wadau wa filamu kuanzisha majumba hayo na ambao tayari wameanzisha kutoa fursa hiyo ili kuziendeleza kazi za filamu za kitanzania.

“Kuwe na majumba ya kuonyeshea sinema ambayo yatakuwa yanazipa kipaumbele filamu za kitanzania”. Alisema Dkt. Fenella.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo alibainisha kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la filamu zinazowasilishwa kwa ukaguzi na pia wadau wameanza kutumia stempu za TRA katika kazi za filamu na muziki ili kuzilinda kazi hizo. Stampu zilianza kutolewa tangu mwezi Januari mwaka huu .

Kwa upande mwingine Mkurugenzi Mkuu Bw. Dileshi Solanki wa Kampuni ya Steps Entertainment ameiahidi Serikali kupitia Waziri wa Habari, Vijana na Utamaduni na Michezo Mhe Dkt Mukangara, kuendelea kuendeleza tasnia ya filamu kwa kushirikiana kikamilifu na serikali na kupiga vita uharamia dhidi ya filamu za kitanzania . Aidha wameiomba serikali kuendelea kuwajengea mazingira mazuri.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3319

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>