Quantcast
Channel: MWINYI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3319

JUA CALI atangaza nia ya kuingia katika Filamu.

$
0
0


Kwa Tanzania tumeshazoea kuona baadhi ya wasanii wa muziki wakiingia katika kuigiza au wa kuigiza wakiingia katika muziki. Mfano mzuri ni Masanja mkandamizaji aliyekua muigizaji wa vichekesho na kuamua kua msanii wa muziki wa injili. Mfano wa pili ni H Baba aliyeamua kuongeza kipato chake kwa kujiingiza katika filamu na bila kusahau watu kama Jay Moe, Ay, TID ambao walikuwaga kwenye Filamu ijulikanayo kama “GIRLFRIEND” ambayo ilitokaga miaka ya nyuma kidogo.

Habari mpya kutoka kwa majirani zetu wa Kenya ni kua msanii Jua Cali ameamua kutangaza wazi kua ana nia ya kuanza kua muigizaji. Jua Cali anayeamba na wimbo wake unaoitwa “Baba Yao” aakihojiwa na redio moja nchini kwao alisema “Me naona mbali you know? Miaka tano ijayo najiona nikiingia katika sector ya movies. Nimekuwa nikitaka kuingia katika sector hii ya filamu tangu zamani. Sababu naamini ukiwa creative wa kutosha waeza fanya chochote”
 
   Asante kwa kutembelea Mwinyi Blog, naomba ubonyeze HAPA ulike page yangu ya facebook ili uendelee kupata matukio mbalimbali ya hapa na pale.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3319

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>