Quantcast
Channel: MWINYI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3319

Jaguar na Julian kutoka Kenya wajitolea kuwasaidia wasanii waliothirika na madawa ya kulevya.

$
0
0




Wasanii wawili Jaguar na Juliani wote kutoka nchini Kenya wameamua kuungana na kuwasaidia wasananii wenzao waliojiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya. Kwa kuanzia wameamua kumsaidia msanii mmoja wa kundi moja maarufu la muziki nchini humo lijulikanalo kama Dandora.

Jaguar na Juliani waliguswa baada ya kumuona msanii huyo akiwa gerezani siku chache zilizopita wakati Jaguar akishoot video ya wimbo wake uitwao Matapeli. Kwa bahati mbaya msanii huyo anaefahamika kwa jina la Johnny Vigetti alitoka gerezani siku hiyo hiyo Jaguar aliyokua akishoot video yake.

Juliani akiongelea swala hilo alisema “tunajaribu kumsaidia Vigetti kuachana na madawa ya kulevya, Tarartibu zote zinafanyika ili aweze kupelekwa Rehab. Tatizo kubwa tulilonalo ni jinsi tunavyoweza kumpata kwani kwa njia ya simu hapatikani.”
 
 Asante kwa kutembelea Mwinyi Blog, naomba ubonyeze HAPA ulike page yangu ya facebook ili uendelee kupata matukio mbalimbali ya hapa na pale.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3319

Trending Articles