Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Serikali imetakiwa kufuatilia mauaji ambayo yamekuwa yakijitokeza hivi karibuni Mkoani Dodoma na kusababisha vifo kwa watu wasiokuwa na hatia.
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Chilonwa Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma Mh. Ezekieli Chibulunje alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Ngomai Wilayani Kongwa waliojikusanya kwa ajili ya kuaga miili ya watu waliopoteza uhai kutokana na mgogoro uliojitokeza Wilayani hapo kati ya wakulima na wafugaji.
Akizungumzia suala hilo Mh. Chibulunje amesema serikali inatakiwa kutoa tamko kutokana na vurugu hizo zilizosababisha mauaji kwani taarifa wanazo na wameahidi wananchi kuwa watazifuatilia.
Nae Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugaia mewapa pole wananchi wote ambao wamepatwa na msiba huo uliotokana na vurugu kati ya wakulima na wafugaji, na kusema kuwa jukumu la kiongozi ni kuhakikisha wanachi wake wakiwa salama vinginevyo kiongozi huyo hafai kuongoza wananchi.
Pia ametoa wito kwa waziri mkuu kutembelea Wilaya ya Kongwa Kijijini hapo ili kujionea mwenyewe mgogoro unaoendelea ili kubaini ukweli uliopo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bwana Peter Msovela ameseama kutokana na mauaji yaliyojitokeza Wilayani hapo, serikali haiwezi kuvumilia mauaji haya yaliyotokea itayashughulikia na kuwachukulia hatua stahili watu watakao bainika.
Watu waliopoteza maishani bwana Emanuel Paul Manyaji mwenye umri wa miaka 40, mgogo alikuwa mchungaji wa kiroho mkazi wa Kijiji cha Ngomai, pamoja na Shukuru Emanuel mwenye umri wa miaka 13 ambae ni mtoto wa bwana Emanuel Mayanji.

Mbunge wa Chilonwa Wilayani Chamwino Mh. Ezekieli Chibulunje akiongea na wananchi wa Kijiji cha Ngomai Wilayani Kongwa Dodoma wakati wa kuaga miili ya watu waliouawa kutokana na Mgogoro wa wakulima na wafugaji.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Peter Msovela akiongea na wakazi wa kijiji cha Ngomai wakati wa mazishi ya watu waliouawa kufuatia mgogoro wa wakulima na wafugaji.
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mh. Job Ndugai kiongea na wananchi wa Kijiji cha Ngomai Wilayani Kongwa Dodoma wakati wa kuaga miili ya watu waliouawa kutokana na Mgogoro wa wakulima na wafugaji.
Wananchi wa Kijiji cha Ngomai Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma wakati wa kuaga miili ya watu hao.
Asante kwa kutembelea Mwinyi Blog, naomba ubonyeze HAPA ulike page yangu ya facebook ili uendelee kupata matukio mbalimbali ya hapa na pale.