













Siku ya juzi majira ya saa moja jioni Mjomba amedhihilisha wazi kwa jamii kuwa kazi anayofanya ni ya uhakika na inalipa baada ya kuizindua Studio yake ya ‘Waite Records’.
Uzinduzi huo uliendana sambamba na utambulisho wa wimbo wake mpya wa ‘Waite’ aliyoutengenezea katika studio yake mtayarishaji akiwa Allan Mapigo.
Mgeni rasmi alikuwa Meya Mstahiki wa Manispaa ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Yusuf Mwenda na baadhi ya wageni waalikwa.
Mjomba aliwashukuru sana watu binafsi na media zinazoendelea kum-support katika kazi zake za muziki hapa Tanzania.
Awali ya yote alitoapongezi kwa Wasanii wote na wadau wanao-support wasanii katika muziki.
SOURCE: BaabKubwa Magazine
Asante kwa kutembelea blog yangu, naomba ubonyeze HAPA ulike page yangu ya facebook ili uendelee kupata matukio mbalimbali ya hapa na pale.