Kama viungo vya ndugu zetu albino ni utajili basi wao ndiyo wangekuwa mabilionea wa kutupa hapa nchini. Acha mawazo finyu IMETOSHA. Albino ni binadamu na kiumbe kama wewe tupige vita mauaji ya albino. Tumuunge mkono ndugu yetu na rafiki, Henry Mdimu ambaye amejitolea kuwa balozi wa kampeni za kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini. Ndugu zetu albino wamenyanyasika sana, wamebezwa, wamekebehiwa sana na sasa tushirikiane naye kwa sauti moja kusema IMETOSHA!! Thank you for visiting Mwinyi Blog, please click HERE to like my facebook page for more entertainment.
↧