Quantcast
Channel: MWINYI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3319

Kili Music Tour Ilivyoiteka Dodoma

$
0
0
Mwishoni mwa wiki ilikuwa zamu ya wakazi wa makao makuu ya nchi kuishuhudia ziara ya wasanii waliofanya vizuri nchini kwa kipindi cha mwaka 2013/2014 maarufu kama Kilimanjaro Music Tour. Ziara hiyo iliwakutanisha wasanii takribani 10 ambao walitoa burudani kwa maelfu ya wakazi wa Dodoma waliofurika katika uwanja wa Jamhuri kushuhudia tamasha hilo ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu. Hizi ni baadhi ya picha za kilichojiri uwanja wa Jamhuri.
Malkia wa mipasho nchini Khadija Kopa aliifungua Kili Music Tour mkoani Dodoma.

Izzo Bizness na Joh Makini katika backstage
 Mwasiti akiendeleza burudani kwa wakazi wa Dodoma ikiwa ni pamoja na kuimba na mmoja ya mashabiki
Rich Mavoko na madansa wake wakilishambulia jukwaa la Kili Music Tour Dodoma
MwanaFA na Anna Peter wakiwa backstage
 Christian Bella “Rais wa Masauti” akiwaimbisha mashabiki uwanja wa Jamhuri
Shilole akiwadhihirishia mashabiki kwa nini anaitwa mtaalam wa jukwaa
 Umati wa mashabiki ukiendelea kufuatilia tamasha
Izzo Bizness alikuwa msanii wa kwanza wa Hip Hop kupanda jukwaani uwanja wa Jamhuri
 Hamis Mwinjuma “MwanaFA” akiendeleza burudani ya Hip Hop katika Kili Music Tour Dodoma.
Wadau wakifurahia kilichokuwa kikiendelea jukwaani
 Ben Pol akiwaburudisha mashabiki wa mkoa ambao alianzia shughuli za muziki
 Shangwe kwa Ben Pol
Weusi wakiikamilisha Kili Music Tour Dodoma kwa show kali

 Thank you for visiting Mwinyi Blog, please click HERE to like my facebook page for more entertainment

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3319

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>