
Mabeste anatarajia kuzindua Documentary ya maisha yake ndani ya Club Billiacanas Jumapili hii. Katika uzinduzi wa documentary hiyo Mabeste atasindikizwa na wasanii wengine kama Country Boy, Queen Darlin, Stamina, Suma Mnazaleti, Deddy, Leo, MRap na wengineo
Akizungumzia Documentary hiyo Mabeste alisema “Ducumentary hiyo mpaka sasa ina dakika zaidi ya 40, na nitakuwa nikiizindua kwa episod, so episod ya kwanza nitaizingua pale Billcanas jumapili hii, na nitaendela na episod zingine katika kumbi zingine.” Mabeste aliongeza kuwa Kwasababu maisha hayasimami yanaendelea na matukio tunakutana nayo kila siku, so documentary hii itaendelea ku-rekodiwa kadri siku zinavyozidi kuendelea.
Asante kwa kutembelea Mwinyi Blog, naomba ubonyeze HAPA ulike page yangu ya facebook ili uendelee kupata matukio mbalimbali ya hapa na pale.