
Baada ya uchunguzi wa nini kilisababisha ajali iliyochukua uhai wa star wa movie ya ”The Fast and the Furious” Paul Walker na rafiki yake Roger Rodas, hatimaye imekuja kugundulika kua ni mwendo kasi wa gari hiyo. Kwa mujibu wa habari iliyotolewa na mtandao maarufu wa TMZ inasema kua Roger ndio alikua akiendesha gari hiyo na alikua akiendesha kwa mwendo wa kasi sana, kwani hadi wakati gari inapata ajali alikua akiendesha kwa kasi ya km 128 hadi 149 kwa saa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo sababu nyingine iliyosababisha ajali hiyo ni kutumiwa kwa matairi ya gari hiyo kwa muda mrefu. Inasemekana tangu gari hiyo inunuliwe miaka 9 iliyopita haikuwahi kubadilishwa tairi zake jambo ambalo lilichangia kwa kiasi kikubwa gari hilo kupoteza mwelekeo. Pia katika uchunguzi huo iligundulika kua hakuna yeyote aliyekua kalewa katika ajali hiyo.
Marehemu Paul alifariki tarehe 30 November mwaka jana na aliacha mtoto mmoja wa miaka 15.
Asante kwa kutembelea Mwinyi Blog, naomba ubonyeze HAPA ulike page yangu ya facebook ili uendelee kupata matukio mbalimbali ya hapa na pale