Quantcast
Channel: MWINYI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3319

Steve Nyerere aja na Snake Kingdom

$
0
0

Hii ndiyo kazi mpya ya Steve Nyerere itakayosambazwa na Proin Promotions
 
MWENYEKITI wa Bongo Movie Unity (BMU), Steven Mengele 'Steve Nyerere' anajiandaa kuiachia hadharani filamu yake mpya kwa mwaka 2014 iitwayo 'Snake Kingdom'.Akizungumza na MICHARAZO, Steve Nyerere alisema filamu hiyo ya kijamii ameigiza na wakali wenzake kama Chuchu Hans, Mayasa Mrisho, Cathy Rupia, Bi Terry 'Mama Nyamayao' na wengine.

Steve Nyerere alisema filamu hiyo ni ya aina yake na kuwataka mashabiki kujiandaa kupata uhondo mara itakapoachiwa mtaani hivi karibuni chini ya kampuni mpya na inayokuja kwa kasi katika kusambaza kazi za wasanii wa filamu nchini ya Proin Promotions.

Mchekeshaji huyo anayeigiza sauti za viongozi mashuhuri, alisema 'Snake Kingdom' ni filamu iliyozalishwa na kampuni yake iliyowahi kutoa filamu kama 'Mwalimu Nyerere', 'My President', 'My Son', 'Mke Mwema' na nyingine.
 
 Asante kwa kutembelea Mwinyi Blog, naomba ubonyeze HAPA ulike page yangu ya facebook ili uendelee kupata matukio mbalimbali ya hapa na pale

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3319

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>