

Mwanadada SHILOLE aka SHISHI BYBEE anatarajia kutoa wimbo wake mpya kabisa kwa mwaka huu 2014 alioupa jina la CHUNA BUZI. Shilole ambaye ni mwigizaji wa Bongo Movie na pia ni msanii wa Bongo Fleva amesema kuwa anatarajia mambo makubwa sana kwa mwaka huu 2014 kama mungu atamjalia pumzi.
Shilole ambaye bado anatesa na kichupa chake kinachoitwa NAKOMAA NA JIJI amesema CHUNA BUZI nimwendelezo tu wa nyimbo zake lakini mashabiki wake wanaona kama majina anayoyachagua kukaa kwenye nyimbo zake yanaonekana kama anayaimba maisha yake. Wimbo huu mpya ameufanyia pale Mazuu Rec chini ya Producer Mazuu. Ni mwisho wa mwezi huu kitu CHUNA BUZI kitaachiwa. Stay connected with Mwinyi Blog.
Asante kwa kutembelea Mwinyi Blog, naomba ubonyeze HAPA ulike page yangu ya facebook ili uendelee kupata matukio mbalimbali ya hapa na pale.