

Mwanamuziki mkongwe wa miondoko ya R&B kutoka nchini Marekani, R Kelly, anatarajiwa kutua nchini Zimbabwe mwezi wa tano mwaka huu, kwa ajili ya kushiriki katika onyesho kubwa la kimataifa la Usiku wa Muziki huko Harare.

Tamasha hili kubwa pia litahusisha wasanii na wadau wengine wa burudani kutoka nchi 20 tofauti, na linatarajiwa kuanza rasmi tarehe 16 mpaka tarehe 25 mwezi Mei likihusisha maonyesho ya muziki sehemu mbalimbali Jijini Harare.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa R Kelly kutua nchini Zimbabwe na
kutumbuiza, na kwa mujibu wa ratiba, atafanya onyesho katika Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano Harare na katika uwanja wa taifa wa nchi hiyo tarehe 25.
Asante kwa kutembelea Mwinyi Blog, naomba ubonyeze HAPA ulike page yangu ya facebook ili uendelee kupata matukio mbalimbali ya hapa na pale.